Skip to main content

Posts

Showing posts from December, 2019

JE, NI MAANDAMANO GANI MAZURI AMBAYO YATAANDAMANA NA KUJA KWA BWANA?

JE, NI MAANDAMANO GANI MAZURI AMBAYO YATAANDAMANA NA KUJA KWA BWANA? Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. 1 Wathesalonike 4:16 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Angalieni, ni siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi, farijianeni kwa maneno hayo. 1 Wathesalonike 4:17-18 Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami po pote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu. Yohana 17:24

IKIWA KIFO SIO KUJA KWA KRISTO, JE ATAKUJAJE?

IKIWA KIFO SIO KUJA KWA KRISTO, JE ATAKUJAJE? wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni. Matendo ya Mitume 1:11 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Baada ya Yesu kuwaambia watapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yao Roho Mtakatifu na watakuwa mashahidi wake katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao. Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, watu wawili wenye nguo nyeupe wakasimama karibu yao wakawaambia jinsi Yesu atakuja. Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi. Luka 21:27 Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina. Ufunuo wa Yohana 1:7

JE, NI WANGAPI WATAPATA MALIPO WAKATI MWANA WA ADAMU ATAKUJA?

JE, NI WANGAPI WATAPATA MALIPO WAKATI MWANA WA ADAMU ATAKUJA? Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. Mathayo 16:27 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kumfuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, amfuate. Mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yake, ataiona. Je, hatamlipa kila mtu sawasawa na kazi yake? Fadhili ziko kwake Bwana, maana ndiye amlipaye kila mtu sawasawa na haki yake. Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu. Yohana 5:29 Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa h...

NI AHADI GANI INAYOTOLEWA KWA WALE WANAOTAZAMIA KUTOKEA KWA KRISTO?

NI AHADI GANI INAYOTOLEWA KWA WALE WANAOTAZAMIA KUTOKEA KWA KRISTO? Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo; Wafilipi 3:20 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Kristo akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu. Kama vile watu walivyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu. Basi, ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi. Waebrania 10:18 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; Waebrania 12:14

KWA NINI NI MUNGU MWENYE WIVU?

KWA NINI NI MUNGU MWENYE WIVU? Maana hutamwabudu mungu mwingine, kwa kuwa Bwana, ambaye jina lake ni mwenye wivu, ni Mungu mwenye wivu. Kutoka 34:14 Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; Wakolosai 3:5 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Wivu wa Mungu unasababishwa na wewe kutokutenda mapenzi yake, yaani kutokutenda yaliyo mema. Maana maovu ni sawa tu na kuabudu sanamu, na imeandikwa tusiabudu miungu mingine ila yeye tuu Yehova, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Tusiwe vuguvugu; kama baridi kuwa baridi, na kama moto kuwa moto. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, Kumbukumbu la Torati 5:9 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu...

KUHUSU ISHARA ZA WAKATI, KWA NINI KRISTO ALIWAKEMEA WAYAHUDI?

KUHUSU ISHARA ZA WAKATI, KWA NINI KRISTO ALIWASHUTUMU WAYAHUDI? Na asubuhi, mwasema, Leo kutakuwa na dhoruba; kwa maana mbingu ni nyekundu, tena kumetanda. Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wa mbingu; lakini, je! Ishara za zamani hizi hamwezi kuzitambua?] Mathayo 16:3 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Sababu waliweza kutambua hali itakavyokuwa kuutambua uso wa mbingu, na  walikuwa wakimjaribu awaonyeshe ishara itokayo mbinguni. Na kilikuwa kizazi kibaya na cha zinaa kilichotaka ishara, na wala kisingepewa. Na ishara waliyopewa ni ya nabii Yona, ambavyo alikaa tumboni mwa nyangumi siku tatu, na ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokaa siku tatu katika moyo wa nchi. Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wa nchi na mbingu; imekuwaje, basi, kuwa hamjui kutambua majira haya? Na mbona ninyi wenyewe kwa nafsi zenu hamwamui yaliyo haki? Luka 12:56-57

JE, NI ISHARA GANI AMBAYO ISAYA ALIPEWA NA AMBAYO KRISTO ANGEJULIKANA KAMA MASIHI?

JE, NI ISHARA GANI AMBAYO ISAYA ALIPEWA NA AMBAYO KRISTO ANGEJULIKANA KAMA MASIHI? Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli. Isaya 7:14 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume, na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani. Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema, Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi. Mathayo 1:22-23 Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu. Luka 1:35

BADALA YA KUTAFUTA UONGOFU WA ULIMWENGU, NINI YATAKUWA MATUMAINI YA KANISA?

BADALA YA KUTAFUTA UONGOFU WA ULIMWENGU, NINI YATAKUWA MATUMAINI YA KANISA? Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; 2 Timotheo 4:7 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Tutalitazamia tumaini lenye baraka na kuonekana kwa utukufu wa Mungu mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo, kwa kumaliza mwendo tukiilinda imani, na tukiwa tumevipiga vita vilivyo vizuri. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. 1 Wathesalonike 4:17 Na Mchungaji mkuu atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya utukufu, ile isiyokauka. 1 Petro 5:4 Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo; ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu. Wafilipi 3:20, Warumi 5:2

JE, BWANA HATAPEWA WATU WA MATAIFA KUWA URITHI?

JE, BWANA HATAPEWA WATU WA MATAIFA KUWA URITHI? Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, Na miisho ya dunia kuwa milki yako. Zaburi 2:8 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Alimuweka awe mfalme, na aihuburi amri, maana ndiye mwanawe aliyemzaa. Yesu Kristo alimtukuza Mungu hapa duniani, hali aliimaliza kazi ile aliyopewa aifanye. Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa. Danieli 7:14 Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako. Yohana 17:5

JE, WALE AMBAO WAPO GIZANI WATASEMA NINI WANAPOSIKIA JUU YA KUJA KWA BWANA?

JE, WALE AMBAO WAPO GIZANI WATASEMA NINI WANAPOSIKIA JUU YA KUJA KWA BWANA? Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe, na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa. 2 Petro 3:3-4 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Ndugu, tuyakumbuke maneno hayo yaliyonenwa zamani na mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba, wakati wa mwisho watakuwako watu wenye kudhihaki, wakifuata tamaa zao wenyewe za upotevu, waletao matengano, watu wa dunia hii tu, wasio na Roho, wenye tabia ya asili wasiopokea mambo ya Roho wa Mungu. Wasema, Na afanye haraka, aihimize kazi yake, tupate kuiona; na likaribie shauri lake aliye Mtakatifu wa Israeli, tupate kuliona. Isaya 5:19 Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia; bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyod...

JE, KUTAKUWA NA AINA NGAPI ZA WATU DUNIANI WAKATI BWANA ATAKAPOKUJA?

JE, KUTAKUWA NA AINA NGAPI ZA WATU DUNIANI WAKATI BWANA ATAKAPOKUJA? Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza. 1 Wathesalonike 5:5 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Ndugu, kwa habari ya nyakati na majira mnajua siku ya Bwana yaja kama mwivi ajavyo usiku. Wasemapo kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo ghafula, kama vile uchungu umjiavyo mwenye mimba, wala hawataokolewa. Basi wa mchana tuendelee kufarijiana na kujengana kila mtu na mwenzake, hivyo hivyo kama tunavyofanya. Zamani tulikuwa giza, bali sasa tumekuwa  nuru katika Bwana, tuenende kama watoto wa nuru; kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli, tukihakiki ni nini impendezayo Bwana. Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku. Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu. 1 Wathesalonike 5:7-8

JE, KATIKA MFANO WAKE WA NGANO NA MAGUGU, MWOKOZI WETU YESU KRISTO ALISEMA NINI?

JE, KATIKA MFANO WAKE WA NGANO NA MAGUGU, MWOKOZI YESU KRISTO ALISEMA NINI? Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu. Mathayo 13:30 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Alifananisha Ufalme wa mbinguni na mtu aliyepanda mbegu njema ya ngano katika konde lake, na baadae watu walipolala akaja adui akapanda magugu katikati yake. Watumwa wa mwenye shamba huyo walitaka kwenda kukusanya magugu yale, ila aliwakataza wasikusanye wakazing'oa ngano pamoja nayo. Akajibu, akasema, Azipandaye zile mbegu njema ni Mwana wa Adamu; lile konde ni ulimwengu; zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni wana wa yule mwovu; yule adui aliyeyapanda ni Ibilisi; mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika. Mathayo 13:37-39

JE, WANAOMTUMIKIA BWANA WATAKUWA KATIKA HALI GANI KABLA BWANA ATAKAPOKUJA?

JE, WANAOMTUMIKIA BWANA WATAKUWA KATIKA HALI GANI KABLA BWANA ATAKAPOKUJA? Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa. 2 Timotheo 3:12 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Roho za wanafunzi zilifanywa imara na kuonywa wakae katika ile imani, sababu iliwapasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi. Bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao; na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu. 2 Timotheo 3:14-15

JE, HALI YA MAISHA ITAKUWA MBAYA KABLA BWANA ATAKAPOKUJA?

JE, HALI YA MAISHA ITAKUWA MBAYA KABLA BWANA ATAKAPOKUJA? lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika. 2 Timotheo 3:13 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Ndivyo nyakati za mwisho ulimwengu hautakuwa na nafuu, hali itazidi kuwa mbaya kabla ya kuja Kristo. Wengine watajitenga na imani kwa kusikiliza roho zidanganyazo na mafudisho ya mashetani. Zitakuwa nyakati za hatari. Watayakataa mafundisho yeye uzima na kufuata nia zao wenyewe wakijipatia waalimu makundi makundi, watajiepusha wasisikie yaliyo kweli kwa kugeukia hadithi za uongo, kwa kuwa wana masikio ya utafiti. Nawaambia, atawapatia haki upesi; walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani? Luka 18:8

JE, NI SIFA GANI ZITAONEKANA HASA KATIKA NYAKATI ZA MWISHO?

JE, NI SIFA GANI ZITAONEKANA HASA KATIKA NYAKATI ZA MWISHO? Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. 2 Timotheo 3:1 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu; wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao. Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; 1 Timotheo 4:1 mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani. Wafilipi 3:19 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate aki...

JE, TUNAWEZA KUJUA SIKU NA SAA YA KUJA KWAKE MWANA WA ADAMU?

JE, TUNAWEZA KUJUA SIKU NA SAA YA KUJA KWAKE MWANA WA ADAMU? Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake. Mathayo 24:36 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Kwa habari ya kuja kwake Mwana wa Adamu, ni Baba peke yake aijuae siku ile na saa ile. Inafananishwa na siku za Nuhu; ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu, watu hawakutambua, ikaja Gharika ikawachukua wote. Watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa. Kesheni maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana. Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie. Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku. 1 Wathesalonike 5:1-2 Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja. Mathayo 24:44

JINSI MITI INAVYOCHIPUA NA KUCHANUA MAJANI, TUJIFUNZE NINI?

JINSI MITI INAVYOCHIPUA NA KUCHANUA MAJANI, TUJIFUNZE NINI? Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu; Mathayo 24:32 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Wakati miti inachipuka na kuchanua majani yake, unatambua kuwa wakati wa mavuno u karibu. Vivyo hivyo tuonapo dalili zote alizotufundisha Kristo Yesu, tutambue kuwa yu mlangoni. Na akatuambi kizazi hiki hakitapita, hata yote yatakapotimia, akimaanisha kizazi kitakachoona dalili hizo za ule mwisho. nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni. Mathayo 24:33 Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. Luka 17:34 Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe. Mathayo 24:35

JE, INJILI INAPASWA KUHUBIRIWA KWA KIWANGO GANI KABLA YA ULE MWISHO?

JE, INJILI INAPASWA KUHUBIRIWA KWA KIWANGO GANI KABLA YA ULE MWISHO? Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja. Mathayo 24:14 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Wengi watajikwaa, nao watasalitiana na kuchukiana, na makristo wa uongo na manabii wengi wa uongo watatokea wakidanganya wengi, wakitoa ishara kubwa na maajabu, wakiwapoteza hata wale wateule, na kuongezeka maasi yatakayosababisha upendo kupoa. Hapo pia injili (habari njema ya ufalme) ya kweli itahubiriwa katika ulimwengu wote na kuwa ushuhuda kwa mataifa yote. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. Mathayo 28:19-20 Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampen...

JE, YESU ALIWAAMBIA WANAFUNZI KUWA ULE MWISHO ULIKUWA KARIBU WAKATI HUO?

JE, YESU ALIWAAMBIA WANAFUNZI KUWA ULE MWISHO ULIKUWA KARIBU WAKATI HUO? Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado. Mathayo 24:6 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Yesu aliwaambia waangalie mtu asiwadanganye, maana wengi watakuja na watadanganya kwa jina lake. Mengi yatatokea lakini ule mwisho bado. Taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na matetemeko ya nchi mahali mahali. Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu. Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi. Mathayo 24:5 Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo. Yohana 5:43

WALIPOSIKIA KRISTO AKISEMA WAKATI UTAFIKA HEKALU LA YERUSALEMU LITAHARIBIWA KABISA, WANAFUNZI WALIMWULIZA NINI?

WALIPOSIKIA KRISTO AKISEMA WAKATI UTAFIKA HEKALU LA YERUSALEMU LITAHARIBIWA KABISA, WANAFUNZI WALIMWULIZA NINI? Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia? Mathayo 24:3 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Baada ya Kristo kuwaambia wanafunzi hawatamuona tena tangu wakati huo, na kuwaambia halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa kwenye majengo ya hekalu la Yerusalemu, wanafunzi walitaka kujua ni lini mambo hayo yatakuwa, na dalili ya kuja kwake na ya mwisho wa dunia. Haya mnayoyatazama, siku zitakuja ambapo halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa. Wakamwuliza wakisema, Mwalimu, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini ishara ya kuwa mambo hayo ya karibu kutukia? Luka 21:6-7

NI AHADI GANI MAALUM, AMBAYO MWOKOZI ALITOA KUHUSU KUJA KWAKE TENA?

NI AHADI GANI MAALUM, AMBAYO MWOKOZI ALITOA KUHUSU KUJA KWAKE TENA? Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. Yohana 14:2-3 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Yesu ndiye njia, na kweli, na uzima, mtu haendi kwa Baba ila kwa njia ya yeye. Amwaminie yeye na kazi alizozifanya, huyo atazifanya, na kubwa kuliko hizo atafanya. Tumwamini Mungu, na tumuamini yeye (Kristo Yesu), tusifadhaike mioyoni mwetu. Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. Yohana 14:13,23

JE, PETRO ALITHIBITISHA VIPI MAHUBIRI YAKE YA ZAMANI KUHUSU KUJA KWAKE KRISTO?

JE, PETRO ALITHIBITISHA VIPI MAHUBIRI YAKE YA ZAMANI KUHUSU KUJA KWAKE KRISTO? Maana hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, tulipowajulisha ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake; bali tulikuwa tumeuona wenyewe ukuu wake. 2 Petro 1:16 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Yesu Kristo alipata heshima na utukufu kutoka kwa Mungu Baba, kwa sauti iliyotoka katika utukufu mkuu, "HUYU NI MWANANGU, MPENDWA WANGU, NINAYEPENDEZWA NAYE". Sauti hiyo waliisikia ikitoka mbinguni walipokuwa naye (Yesu Kristo) katika mlima ule mtakatifu. Msikilizeni yeye. Alipokuwa katika kusema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye. Mathayo 17:5 Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing'aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka m...

MANABII WA UONGO, MSIJALI, ENDELEENI NA HUO UONGO WENU.

MANABII WA UONGO, MSIJALI, ENDELEENI NA HUO UONGO WENU. Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Ninyi manabii wa uongo, msiache, endeleeni, maana hamtakamatwa, tena msisahau Wakristo ni wepesi wa kusahau hayo mnayoyasema. Tena maandiko yanawaonya wasitweze unabii. Hivyo nyie endeleeni, hawataudharau unabii. Ila mkumbuke wanaopokea huo unabii (watu wa Mungu na watoto wa Mungu) wameambiwa kwenye maandiko, wafurahi sikuzote, wakiomba bila kukoma na wakishukuru kwa kila jambo, maana hayo ndiyo mapenzi ya Mungu kwetu katika Kristo. Na pia wasimzimishe Roho, wakijaribu mambo yote kwa kuyashika yaliyo mema, pamoja na kujitenga na ubaya wa kila namna. Watu wa Mungu hawaangamii, bali wanangamizwa kwa kukosa maarifa, kwa kuwa wewe kuhani umeyakataa maarifa. Lakini watoto wa Mungu wanayatafuta na wanayo maarifa, watawashtukia tuu uongo wenu, maana mnafahamika mpo kila mahali. Hosea 4:6 na 1 Wathesalonike 5:16-23 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni h...

KATIKA KUTOA UTABIRI WA KINABII, MANABII WALITAFUTA NINI?

KATIKA KUTOA UTABIRI WA KINABII, MANABII WALITAFUTA NINI? Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi. 1 Petro 1:10 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Katika kupokea wokovu wa roho zetu, twampenda Yesu Kristo ijapokuwa hatukumwona na hatumwoni hata sasa, twamwamini na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka yenye utukufu. Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo. 1 Petro 1:11 Kwa maana, amin, nawaambia, Manabii wengi na wenye haki walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi, wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi, wasiyasikie. Mathayo 13:17

JE, NI NINI KISEMWACHO JUU YA TAFSIRI YA UNABII?

JE, NI NINI KISEMWACHO JUU YA TAFSIRI YA UNABII? Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. 1 Wakorintho 2:13 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Tumshukuru Mungu siku zote kwa neema aliyotupa katika Kristo Yesu. Hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho wa Mungu ili tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. Mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. 2 Petro 1:20

JE, UNABII KWENYE WA AGANO LA KALE TUMEPEWAJE?

JE, UNABII WA AGANO LA KALE TUMEPEWAJE? Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu. 2 Petro 1:21 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Unabii uliletwa kwa wanadamu kunena walivyoongozwa na Roho Mtakatifu. Hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani. Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini. Warumi 15:4 Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani. 1 Wakorintho 10:11

JE, KITABU CHA MWISHO KWENYE BIBLIA KINAITWAJE, NA NINI KINASEMWA KWA ANAYESOMA AU KUJIFUNZA KITABU HIKI?

JE, KITABU CHA MWISHO KWENYE BIBLIA KINAITWAJE, NA NINI KINASEMWA KWA ANAYESOMA AU KUJIFUNZA KITABU HIKI? Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana; Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu. Ufunuo wa Yohana 1:1,3 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Ni Ufunuo wa Yesu Kristo kwa mtumwa wake, Yohana, aliopewa na Mungu kwa ajili ya kuwaonyesha watumwa wa Kristo mambo ambayo hayana budi kuwako upesi. Amebarikiwa anayeyasoma, asikiaye na kuyashika maneno yaliyoandikwa kwenye unabii huu, kwa maana wakati u karibu. Na tazama, naja upesi; heri yeye ayashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki. Akaniambia, Usiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia. Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi ...

JE, MAMBO YALIYOFUNULIWA NI KWA AJILI YA NANI?

JE, MAMBO YALIYOFUNULIWA NI KWA AJILI YA NANI? Mambo ya siri ni ya Bwana, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno yote ya sheria hii. Kumbukumbu la Torati 29:29 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Sheria ya Bwana ni kamilifu, huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa Bwana ni amini, humtia mjinga hekima. Mtu mkaidi ni chukizo kwake, bali siri yake ni pamoja na wanyofu. Tuwe waungwana tukilipokea neno kwa uelekevu, kwa kuyachunguza maandiko kila siku, kwa maana yamefunuliwa kwa familia ya wanadamu milele. Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake. Amosi 3:7 Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. Yohana 5:39 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata m...

NI KWA NJIA GANI KILA ANDIKO LILITOLEWA NA KWA KUSUDI GANI?

NI KWA NJIA GANI KILA ANDIKO LILITOLEWA NA KWA KUSUDI GANI? Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema. 2 Timotheo 3:16-17 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Ili mtu wa Mungu awe kamili na apate kutenda matendo mema, kila andiko lenye pumzi ya Mungu lamfaa kumfundisha, kumuonya makosa yake, kumuongoza na kumuadabisha katika haki. Mtu wa Mungu uyakimbie mabaya, ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, saburi, upole. Tuwafundishe watu kuyakubali maneno yenye uzima ya Bwana wetu Yesu Kristo, mafundisho yapatanayo na utauwa. Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini. Warumi 15:4 Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiong...

JE, NI VIPI MUNGU AMELIKUZA NENO LAKE?

JE, NI VIPI MUNGU AMELIKUZA NENO LAKE? Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu, Nitalishukuru jina lako, Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako, Kwa maana umeikuza ahadi yako, Kuliko jina lako lote. Zaburi 138:2 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Tunapaswa, basi, kulipitia Neno la Mungu kwa heshima kubwa, na kuchunguza kurasa zake kila siku, ili tuweze kujifunza zaidi juu ya Mungu. Tulisikie neno lake na kulitia moyoni. Bwana akapendezwa, kwa ajili ya haki yake, kuitukuza sheria, na kuiadhimisha. Isaya 42:21 Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni. Mathayo 10:32

JE, NI NINI MTU ANAHITAJI ILI AISHI?

JE, NI NINI MTU ANAHITAJI ILI AISHI Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu. Mathayo 4:4 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Mtu anatakiwa apate chakula cha mwili na pia anatakiwa sana apate Neno La Mungu kama chakula cha kiroho ili aishi. Kama mtu anaishi kwa Neno la Mungu, anapaswa lazima kulitumia kila siku  kwani ni lishe ya kila siku inayohitajika kumweka hai. Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo. Matendo ya Mitume 17:11 Akakutweza, akakuacha uone njaa, akakulisha kwa mana, usiyoijua wewe wala baba zako hawakuijua; apate kukujulisha ya kuwa mwanadamu haishi kwa mkate tu, bali huishi kwa kila litokalo katika kinywa cha Bwana. Kumbukumbu la Torati 8:3