Skip to main content

Posts

Showing posts from November, 2019

JE, MAANDIKO YANA UWEZO WA KUKUFANYIA NINI?

JE, MAANDIKO YANA UWEZO WA KUKUFANYIA NINI? na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu. 2 Timotheo 3:15 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Ili mtu wa Mungu awe kamili na apate kutenda matendo mema, kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa kufundisha, kumuonya mtu makosa yake, kumuongoza na kumuadabisha katika haki. Watu hawana neno la Mungu likakaa ndani yao, kwa sababu hawamwamini yule aliyetumwa na yeye. Mwamini yule aliyetumwa (Kristo Yesu) ndipo uyachunguze maandiko. Bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao; 2 Timotheo 3:14 lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika. 2 Timotheo 3:13 Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote, Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo. Zaburi 119:99

JE, NI MAELEZO YA KWELI KWAMBA AGANO JIPYA LILIFICHWA KWENYE LA KALE, NA AGANO LA KALE LIMEFUNULIWA KWENYE JIPYA?

JE, NI MAELEZO YA KWELI KWAMBA AGANO JIPYA LILIFICHWA KWENYE LA KALE, NA AGANO LA KALE LIMEFUNULIWA KWENYE JIPYA? Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, Je! Yamekuelea haya unayosoma? Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye. Matendo ya Mitume 8:30-31 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Ni ukweli kabisa Agano la Jipya lilifichwa kwenye la Kale, na Agano la Kale limefunuliwa kwenye Jipya. Ni kwa uwazi kabisa unaoonekana, Kristo amejulikana katika maandiko ya Agano la Kale. Bila Agano la Kale habari za Kristo kuwa ndiye Masihi zisingeimarika. Tusingependa kujifunza  Biblia yote, kama Wayahudi, tungepoteza muelekeo wa vitu muhimu sana  vilivyomo kwenye Agano Jipya lenyewe. Yule towashi akamjibu Filipo, akasema, Nakuomba, nabii huyu; asema maneno haya kwa habari ya nani; ni habari zake mwenyewe au za mtu mwingine? Filipo akafunua kinywa chake, naye, ...

JE, NINI LILIKUWA JIWE KUU LA MSINGI WA IMANI YA MITUME NA MANABII?

JE, NINI LILIKUWA JIWE KUU LA MSINGI WA IMANI YA MITUME NA MANABII? Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Waefeso 2:20 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Yeye (Kristo Yesu) ndiye kichwa, ambacho kwa yeye mwili wote kwa viungo na mishipa umeunganishwa, na hukua kwa maongeo yatokayo kwa Mungu. Na katika yeye jeng lote limeunganishwa vyema na kukua hata liwe hekalu takatifu la Mungu. kwa ajili ya hayo Bwana, MUNGU, asema hivi, Tazama, naweka jiwe katika Sayuni, liwe msingi, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni lenye thamani, msingi ulio imara; yeye aaminiye hatafanya haraka. Isaya 28:16 Kwa maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba katika Roho mmoja. Waefeso 2:18

WAISRAELI WALIPATA WAPI CHAKULA NA KINYWAJI CHA ROHO WALIPOKUWA JANGWANI?

WAISRAELI WALIPATA WAPI CHAKULA NA KINYWAJI CHA ROHO WALIPOKUWA JANGWANI? wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari; wote wakala chakula kile kile cha roho; wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo. 1 Wakorintho 10:2-4 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Lakini pamoja na hayo wengi hawakumpendeza Mungu na waliangamizwa jangwani. Mambo haya yalikuwa mfano kwetu ili tusiwe wa kutamani mabaya kama wale walivyotamani. Yaliandikwa kwa jinsi ya mifano ili kutuonya sisi. Tazama, nitasimama mbele yako huko, juu ya lile jabali katika Horebu; nawe utalipiga jabali, na maji yatatoka, watu wapate kunywa. Musa akafanya hivyo mbele ya wazee wa Israeli. Kutoka 17:6 Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke. Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani. 1 Wakorintho 10:20-21

KWA NINI MUSA ALIACHA UTAJIRI WA MISRI?

KWA NINI MUSA ALIACHA UTAJIRI WA MISRI? akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo. Waebrania 11:26 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Kwa imani Musa alipokuwa mtu mzima alikataa kuitwa mwana wa binti Farao akaona ni afadhali kupata mateso na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa muda. Ee Bwana, ukumbuke, Wanavyosimangwa watumishi wako; Jinsi ninavyostahimili kifuani mwangu Masimango ya watu wengi. Zaburi 89:50

JE, ILIKUWA INJILI YA KRISTO ILIYOHUBIRIWA KWA IBRAHIMU, NA HABARI NJEMA IMEHUBIRIWA WAKATI WA AGANO LA KALE?

JE, ILIKUWA INJILI YA KRISTO ILIYOHUBIRIWA KWA IBRAHIMU, NA HABARI NJEMA IMEHUBIRIWA WAKATI WA AGANO LA KALE? Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi. Yohana 8:56 Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia. Waebrania 4:2 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Vile vile kama hao ni Waisraeli wakati wa safari yao kutoka Misri kuelekea nchi ya ahadi. Maandiko yanatuambia tumehubiriwa habari njema kama wao, hivyo tunaposikia habari njema tusifanye migumu mioyo yetu. Basi, kwa kuwa neno hili limebaki kwamba wako watu watakaoingia humo, na wale waliohubiriwa habari ile zamani walikosa kuingia kwa sababu ya kuasi kwao, Waebrania 4:6

JE, KUNA KUMBUKUMBU YOYOTE YA HABARI NJEMA KUHUBIRIWA MAPEMA?

JE, KUNA KUMBUKUMBU YOYOTE YA HABARI NJEMA KUHUBIRIWA MAPEMA? Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani, lilimhubiri Ibrahimu habari njema zamani, kusema, Katika wewe Mataifa yote watabarikiwa. Wagalatia 3:8 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Mungu alimuahidi kumfanya Abramu kuwa taifa kubwa, kumbariki, kulikuza jina lake, na awe baraka. Na watakaombariki watabarikiwa, na watakaomlaani watalaaniwa na katika yeye jamaa zote za dunia zitabarikiwa. akiwa Ibrahimu atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa? Mwanzo 18:18

JE, WEWE NI WA ULIMWENGU HUU?

JE, WEWE NI WA ULIMWENGU HUU? Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu. Warumi 12:2 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Tumezaliwa mara ya pili, tumekuwa kiumbe kipya, tumezaliwa na Mungu. Tuuvue mwenendo wa kwanza utu wa zamani unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya, na tufanywe upya katika roho ya nia zetu. Kwa hivyo, tusiwe wajinga, bali tufahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana. PAMOJA TUNAISHI KATIKA ULIMWENGU HUU, SISI SI WA ULIMWENGU HUU. ambaye alijitoa nafsi yake [Yesu Kristo] kwa ajili ya dhambi zetu, ili atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama alivyopenda Mungu, Baba yetu. Wagalatia 1:4 mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli. Waefeso 4:24 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. 2 Wakorintho 5:17 ...

FANYENI YOTE KWA MOYO, MKIMSHUKURU MUNGU.

FANYENI YOTE KWA MOYO, MKIMSHUKURU MUNGU. Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu, mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo. Wakolosai 3:24 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Unapofanya jambo, fanya kwa upendo ukijua kabisa unafanya kwa ajili ya Mungu wala si kwa wanadamu. Ukihudumu, ukiomba, ukitoa, na yote fanya kwa moyo ukijua unamtumikia Bwana na utapokea ujira kwa Bwana. Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu; 1 Petro 2:2 Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye. Wakolosai 3:17

KAMA VIUNGO KATIKA MWILI WA KRISTO, NINI WAJIBU WA KILA MMOJA?

KAMA VIUNGO KATIKA MWILI WA KRISTO, NINI WAJIBU WA KILA MMOJA? ili kusiwe na faraka katika mwili, bali viungo vitunzane kila kiungo na mwenziwe. 1 Wakorintho 12:25 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile twavipa heshima zaidi; na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uzuri zaidi sana. Kama mwili wote ukiwa jicho, ku wapi kusikia? Kama wote ni sikio ku wapi kunusa? 1 Wakorintho 12:17 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo. Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo. Waefeso 4:11,15,16

JE, MTUME PAULO ALILINGANISHA KANISA NA NINI?

JE, MTUME PAULO ALILINGANISHA KANISA NA NINI? Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake. 1 Wakorintho 12:27 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Mungu ameweka wengi katika kanisa na kila mmoja na karama yake. Viungo ni vingi ila mwili ni mmoja.  Kiungo kimoja kikiumia vyote vimeumia nacho, na kimoja kikitukuzwa vyote hufurahi pamoja nacho. Hivyo, kanisa tu viungo vya mwili wake Kristo. Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja; Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake. Warumi 12:4-5 Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa. Waefeso 5:29

HUU MGAWANYIKO KATIKA KANISA LA MUNGU UMESABABISHA NINI TANGU NYAKATI ZA PAULO?

HUU MGAWANYIKO KATIKA KANISA LA MUNGU UMESABABISHA NINI TANGU NYAKATI ZA PAULO? Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa. Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake; yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo; na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa. Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo; ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu. 2 Wathesalonike 2:7-12 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote, maana atakuja huyo ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu na ataketi katika hekalu la Mungu akijionyesha nafsi yake kana kwamba ndiye Mungu. Maana ...

NINI SABABU YA KWANZA YA MGAWANYIKO KATIKA KANISA LA KRISTO?

NINI SABABU YA KWANZA YA MGAWANYIKO KATIKA KANISA LA KRISTO? Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi; tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao. Matendo ya Mitume 20:29-30 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Katika hao hao waangalizi walioachiwa kanisa la Mungu ndio walipoinuka mbwa mwitu na kulipotosha kundi (wanafunzi) bila huruma, wawafuate wao. Tatizo ni watu kukosa maarifa ndio maana wanaangamizwa. Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe. Matendo ya Mitume 20:28 Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. Mathayo 7:15 Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwa-mwitu anakuja,...

JE, MTUME PAULO ALIFUNDISHA NINI KUHUSU UMOJA?

JE, MTUME PAULO ALIFUNDISHA NINI KUHUSU UMOJA? Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja. 1 Wakorintho 1:10 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Anatufundisha kwamba ndugu katika Kristo Yesu tuenende kwa furaha, tukiwa na nia moja, mapenzi mamoja, wenye roho moja, tukinia mamoja. Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Wafilipi 2:3

JE, KANISA LITAKUWA NA USHAWISHI GANI KWA WASIOAMINI?

JE, KANISA LITAKUWA NA USHAWISHI GANI KWA WASIOAMINI? Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. Yohana 17:21 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Kwa umoja ndani ya kanisa, na Upendo na matendo mema kutashawishi ulimwengu kusadiki kwamba Yesu ni Bwana, na ndiye aliyetumwa na Baba. Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu. Wagalatia 3:28

NI, JAMBO GANI KRISTO ALILOOMBA KWA BABA KWA NIABA YA WANAFUNZI WAKE?

NI, JAMBO GANI KRISTO ALILOOMBA KWA BABA KWA NIABA YA WANAFUNZI WAKE? Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo. Yohana 17:11 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Jambo kuu umoja wao ulilo nao ni UPENDO. Na amri mpya aliyotupa Bwana wetu Yesu Kristo ni tupendane sisi kwa sisi, na tuwe na umoja kama wao walivyo na umoja wenye upendo wa ajabu sana. Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu. Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. Yohana 17:15-21

NI UHUSIANO GANI UNAOENDELEA KATI YA BABA NA MWANA?

NI UHUSIANO GANI UNAOENDELEA KATI YA BABA NA MWANA? Mimi na Baba tu umoja. Yohana 10:30 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Huu ndio uhusiano uliopo kati ya Mungu na mwana wake mpendwa Kristo Yesu. Hakuna alilofanya Bwana wetu Yesu Kristo kwa mapenzi yake mwenyewe, ila aliyoambiwa na Baba aliyemtuma kwetu. Kusudi lao ni moja. Mwana hakushuka kutoka mbinguni ili ayafanye mapenzi yake, ila mapenzi yake Baba aliyemtuma. Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka. Mimi nikijishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu si kweli. Yohana 5:30-31 Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile. Yohana 5:19

AGANO JIPYA LINASEMAJE KUHUSU KINYONGO?

AGANO JIPYA LINASEMAJE KUHUSU KINYONGO? Ndugu, msinung'unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango. Yakobo 5:9 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Wengi wetu tumekuwa tukijifanya tunajua kusamehe kwa kusema " Nisamehe kabisa, lakini sitasahau". Hii ni kushikilia kinyongo. Tuangalie, tusije hukumiwa kwa kujidanganya huku. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu. Mathayo 6:12,14,15 tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi. Waefeso 4:32 mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. Wakolosai 3:13

JE, MUNGU HAKUKATAZA KINYONGO TANGU ZAMANI?

JE, MUNGU HAKUKATAZA KINYONGO TANGU ZAMANI? Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani yako kama nafsi yako; Mimi ndimi Bwana. Mambo ya Walawi 19:18 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Usiwachukie wengine moyoni mwako, wala usichukue dhambi kwa ajili yao. Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni. Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. Warumi 12:17 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu. Mathayo 5:48

KATIKA KUSAMEHE, NI MFANO GANI TUUFUATE?

KATIKA KUSAMEHE, NI MFANO GANI TUUFUATE? Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. Wakolosai 3:12-13 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Tukiwasamehe watu makosa yao, na Baba yetu wa mbinguni atatusamehe makosa yetu, tukichukuliana kwa upendo. tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi. Waefeso 4:32 kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo; Waefeso 4:2

NI JINSI GANI TUNAPASWA KUTOA REHEMA?

NI JINSI GANI TUNAPASWA KUTOA REHEMA? mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha. Warumi 12:8 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Tumepewa karama mbalimbali ikiwemo kurehemu kwa furaha. Pendo lisiwe la kinafiki, tuchukie maovu, tuambatane na yaliyo mema. Tubariki wanaotuudhi wala tusilaani. Tusilipe ovu kwa ovu. Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani. Warumi 12:14 Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. 2 Wakorintho 9:7

KATIKA KUSHUGHULIKA NA MAKOSA, NI HISIA GANI ZINAPASWA KUTUCHOCHEA?

KATIKA KUSHUGHULIKA NA MAKOSA, NI HISIA GANI ZINAPASWA KUTUCHOCHEA? Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi; nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe? Mathayo 18:32-33 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Tusipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yetu hatatusamehe sisi makosa yetu. Bwana wake akaghadhibika, akampeleka kwa watesaji, hata atakapoilipa deni ile yote. Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake. Mathayo 18:34-35 Jilindeni; kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe. Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe. Luka 17:3-4

JE, NI KWA MFANO GANI TULIOFUNDISHWA KUSAMEHE?

JE, NI KWA MFANO GANI TULIOFUNDISHWA KUSAMEHE? Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake. Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talanta elfu kumi. Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile deni. Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia. Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni. Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinari mia akamkamata,akamshika koo,akisema Nilipe uwiwacho. Basi mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia. Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa ile deni. Basi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka. Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile...

TUTAOMBAJE MSAMAHA, NA NI MARA NGAPI TUSAMEHE?

TUTAOMBAJE MSAMAHA, NA NI MARA NGAPI TUSAMEHE? Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Mathayo 6:12 Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba? Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini. Mathayo 18:22 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.  Ukisamehe sahau kabisa, kama mashariki ilivyo mbali na magharibi. Usibaki na chochote moyoni mwako. Msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu. Mathayo 6:14-15

NI ROHO GANI INAPASWA KUONGOZANA NA SALA?

NI ROHO GANI INAPASWA KUONGOZANA NA SALA? Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. Marko 11:25 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Ili Baba yetu wa mbinguni atusamehe inatubidi tuwasamehe watu wote waliotukosea kwanza, na ndipo tusimame na kusali. Roho yako inatakiwa iwe safi, isiwe na neno juu ya mtu yoyote usalipo. Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako. Mathayo 5:23-24 [Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.] Marko 11:26 Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu. Marko 11:24

NI NINI HATMA YA WALE AMBAO WATAONGEZA AU KUPUNGUZA MANENO YA UNABII?

NI NINI HATMA YA WALE AMBAO WATAONGEZA AU KUPUNGUZA MANENO YA UNABII? Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki. Ufunuo wa Yohana 22:18-19 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Usisikilize viongozi wa uwongo ambao wanatafuta faida, usisikilize sauti zao zinazodanganya. Uliza kitabu ha mwongozo, Biblia kutoka Mbinguni; tumepewa kurasa zake kwa ajili ya wokovu wetu, ikiwa unatafuta njia ya kweli. Msiliongeze neno niwaamurulo wala msilipunguze, mpate kuzishika amri za Bwana, Mungu wenu, niwaamuruzo. Kumbukumbu la Torati 4:2 Neno niwaagizalo lo lote liangalieni kulifanya; usiliongeze, wala usilipunguze. Kumbukumbu la Torati 12:32 Na...

JE, BWANA ANASEMA NINI KUHUSU WACHUNGAJI WA UWONGO?

JE, BWANA ANASEMA NINI KUHUSU WACHUNGAJI WA UWONGO? Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea, wachungaji wao wamewapoteza; wamewapotosha milimani; wamekwenda toka mlima hata kilima, wamesahau mahali pao pa kupumzika. Yeremia 50:6 Mwanadamu, toa unabii juu ya wachungaji wa Israeli, toa unabii, uwaambie, naam, hao wachungaji, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wachungaji wa Israeli, wanaojilisha wenyewe; je! Haiwapasi wachungaji kuwalisha kondoo? Mnawala walionona, mnajivika manyoya, mnawachinja walionona; lakini hamwalishi kondoo. Ezekieli 34:2-3 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.  Watu kwa kukosa maarifa ya Neno la Mungu mioyoni mwao wanaangamizwa , wanatangatanga kama kondoo aliyekosa mchungaji. Mtumwa wa Bwana asiwe mgomvi bali mwanana kwa watu wote, aweze kufundisha na awe mvumilivu. Watu wanachukia mema, wanapenda mabaya. Watamwomba Bwana, asiwaitikie, atawaficha uso wake wakati huo wa hukumu, kwa kadri walivyotenda mabaya kwa matendo yao....

JE, NENO LA MUNGU LINASEMA NINI KUHUSU WALIOIJUA NJIA NA HAWATEMBEI NDANI YAKE?

JE, NENO LA MUNGU LINASEMA NINI KUHUSU WALIOIJUA NJIA NA HAWATEMBEI NDANI YAKE? Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa. 2 Petro 2:21 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.  Neno linasema kuijua kweli na njia ya haki, na kuiacha na kurudi na kuendelea ni sawasawa na mbwa aliyerudia matapiko yake na nguruwe aliyeoshwa na kurudi kugaa-gaa matopeni. Unatakiwa kuijua kweli, na hiyo kweli ikuweke huru kweli kweli. Unatakiwa uijue kwa kupata maarifa ili usiangamizwe. Maana watu wa Mungu wanaangamizwa na sacbabu kubwa ni kukosa maarifa, na maarifa utayapata kwa kulisikiliza Neno La Mungu moyoni mwako. Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo. Yuda 1:4 Moyo wa mwenye busara hupata maarifa; Na sikio la mwenye hek...

JE, WANATEGEMEA BWANA KUSIKIA NA KUJIBU MAOMBI YAO?

JE, WANATEGEMEA BWANA KUSIKIA NA KUJIBU MAOMBI YAO? Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria, Hata sala yake ni chukizo. Mithali 28:9 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Itafika wakati watayakataa mafundisho yenye uzima, watazifuata nia zao wenyewe wakijipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti. Lihubiri neno wakati wote, karipia, kemea na onya kwa uvumilivu wote na mafundisho. Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana asingesikia. Hakika Mungu amesikia; Ameisikiliza sauti ya maombi yangu. Zaburi 66:19 Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako. 2 Timotheo 4:5 Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze. Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu. Luka 13:27

JE, KUFUNDISHANA HUKU NA KUABUDU HUKU KUNAKUBALIKA NA BWANA?

JE, KUFUNDISHANA HUKU NA KUABUDU HUKU KUNAKUBALIKA NA BWANA? wawaambiao waonaji, Msione; na manabii, Msitoe unabii wa mambo ya haki, tuambieni maneno laini, hubirini maneno yadanganyayo; Isaya 30:10 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Tatizo kubwa watu wamemkaribia Mungu wakimuabudu, wakimsifu  na kumheshimu kwa vinywa vyao tuu, mbali mioyoni mwao ni mawazo ya kibinadamu iliyofarakana na Mungu, kwa mafundisho na maagizo ya wanadamu. Bwana akanena, Kwa kuwa watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao, bali mioyo yao wamefarakana nami, na kicho chao walicho nacho kwangu ni maagizo ya wanadamu waliyofundishwa; Isaya 29:13 Akawaambia, Isaya alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa, Watu hawa huniheshimu kwa midomo Ila mioyo yao iko mbali nami; Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu, Marko 7:6-7