Skip to main content

Posts

Showing posts from March, 2020

MPINGA KRISTO YUAJA, NA WENGI WAMEKUWEPO.

MPINGA KRISTO YUAJA, NA WENGI WAMEKUWEPO. Neema na amani na ziongezwe kwetu.     Ni wakati wa mwisho, na kama mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja; sio hivyo tuu hata wakati huo walikuwepo. Tumepakwa mafuta na yeye akiye mtakatifu, hivyo tunajua yote. Hatukuandikiwa sisi kwa sababu hatujui iliyo kweli, bali kwa sababu tunaijua, tena hakuna uongo wo wote utokao katika hiyo kweli. Aliye mwongo ni yule akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo; na huyu ndiye mpinga Kristo, amkanaye Baba na Mwana. Basi tulilosikia tangu mwanzo likikaa ndani yetu nasi tutakaa ndani ya Mwana,  na ndani ya Baba.     Kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu, na hii ndio roho ya mpinga Kristo ambayo tumesikia yaja, na sasa tayari imekwisha kuwako duniani. Hivyo tusiamini kila roho, bali tuzijaribu hizo roho kama zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. Twamjua Roho wa Mungu, na kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na ...

UMOJA TULIOITIWA ILI TURITHI BARAKA.

UMOJA TULIOITIWA ILI TURITHI BARAKA. Neema na amani na ziongezwe kwetu.     Tuwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu; watu tusiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo tuliyoitiwa ili turithi baraka. Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila, Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate sana.     Tuwabariki wanaotuudhi; tubariki, wala tusilaani. Tufurahi pamoja nao wafurahio; tulie pamoja nao waliao. Tupatane nia zetu sisi kwa sisi. Tusinie yaliyo makuu, lakini tukubali kushughulishwa na mambo manyonge. Tusiwe watu wa kujivunia akili. Tusimlipe mtu ovu kwa ovu. Tuangalie yaliyo mema machoni pa watu wote. Tukae katika amani na watu wote. Tusijilipize kisasi, bali tuipishe ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.     Maneno yet...

TU WARITHI KWA MUNGU PAMOJA NA KRISTO.

TU WARITHI KWA MUNGU PAMOJA NA KRISTO. Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu katika Kristo Yesu.     Roho wa Mungu anakaa ndani yetu, hivyo hatuufuati mwili, bali tunaifuata roho. Na wote tunaoongozwa na Roho wa Mungu, ndio wana wa Mungu. Hatukupokea tena roho ya utumwa iletayo hofu, bali roho ya kufanywa wana, na kwa hiyo twalia Aba, yaani Baba. Roho  mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu ya kuwa sisi tuu watoto wa Mungu; hivyo kama watoto, tu warithi wa Mungu, turithio pamoja na Kristo, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.     Basi sisi si watumwa tena bali tu wana,  na kama wana tu warithi kwa Mungu. Tulikuwa chini ya sheria, tukakombolewa ili tupate hali ya kuwa wana; na kwa kuwa tumekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye Aba, yaani, Baba. Na kama sisi ni wa Kristo, tumekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.     Mungu hakutupa roho ya woga, b...

UFALME WA MUNGU UMEKARIBIA.

  UFALME WA MUNGU UMEKARIBIA. NEEMA NA IWE KWENU, NA AMANI, ZITOKAZO KWA MUNGU BABA YETU KATIKA KRISTO YESU.     WAKATI UMETIMIA, NA UFALME WA MUNGU UMEKARIBIA; TUBUNI NA KUIAMINI INJILI. UFALME WA MUNGU NI HAKI NA AMANI NA FURAHA KATIKA ROHO MTAKATIFU. UTAFUTENI KWANZA UFALME WA MUNGU NA HAKI YA MUNGU. TORATI NA MANABII VILIKUWAPO MPAKA YOHANA, NA TOKEA WAKATI HUO HABARI NJEMA YA UFALME WA MUNGU HUTANGAZWA, NA KILA MTU HUJIINGIZA KWA NGUVU.     TANGU SIKU ZA YOHANA MBATIZAJI HATA SASA UFALME WA MBINGUNI HUPATIKANA KWA NGUVU, NAO WENYE NGUVU WAUTEKA, MAANA MANABII WOTE NA TORATI WALITABIRI MPAKA WAKATI WA YOHANA, NA YEYE NDIYE ELIYA ATAKAYEKUJA. MWENYE MASIKIO NA ASIKIE. JITAHIDINI KUINGIA KATIKA MLANGO ULIO MWEMBAMBA, KWA MAANA WENGI WATATAKA KUINGIA WASIWEZE.     KWA MAANA HATUKUJA NA KITU DUNIANI, HIVYO HATUWEZI KUTOKA NA KITU. SHINA MOJA LA MABAYA YA KILA NAMNA NI KUPENDA FEDHA, AMBAPO WENGI WAMEFARAKANA NA IMANI KWA KUPENDA HILO...

TUKAE NDANI YAKE, NA YEYE NDANI YETU.

TUKAE NDANI YAKE, NA YEYE NDANI YETU. Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu katika Kristo Yesu.     Katika mfano Kristo Yesu alioutumia hapa, anatuambia yeye ndiye mzabibu wa kweli, na Mungu Baba yetu ndiye mkulima. Na kila tawi ndani yake lizaalo, hulisafisha lizidi kuzaa, bali tawi lisilozaa huliondoa. Sisi tumekwisha kuwa safi kwa neno lake.  Hivyo, tukae ndani yake, na yeye ndani yetu.     Yeye ni mzabibu; sisi ni matawi; tukaao ndani yake naye ndani yetu, twazaa sana maana pasipo yeye sisi hatuwezi kufanya neno lo lote. Tukikaa ndani yake na maneno yake yakikaa ndani yetu, tuombe tutakalo lote nasi tutatendewa.     Kama vile mwili ni mmoja, una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule ni vingi, ni mwili mmoja, vivyo hivyo na Kristo. Kiungo kimoja kikiumia, vyote huumia nacho, au kimoja kikitukuzwa, vyote hufurahi pamoja nacho. Basi tumekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke. Yohana 15:1-7, 1 Wa...

MTAKUWA WATAKATIFU KWA KUWA YEYE NI MTAKATIFU.

MTAKUWA WATAKATIFU KWA KUWA YEYE NI MTAKATIFU. Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu katika Kristo Yesu.     Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki, maana ufalme wa mbinguni ni wao. Tujapoteswa kwa sababu ya haki tuna heri. Tusiogope kutisha kwao wala tusifadhaike , bali tumtakase Kristo Bwana mioyoni mwetu. Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake husikiliza maombi yao. Hakuna wa kutudhuru, tukiwa wenye juhudi katika mema. Tukistahimili tutendapo matendo mema na kupata mateso, huu ndio wema hasa mbele za Mungu.     Tumjibu kila mtu habari za tumaini lililo ndani yetu, kwa upole na kwa hofu. Tuwe na dhamiri njema, ili lile neno tunalosingiziwa, watahayarishwe wale wautukanao mwenendo wetu mwema katika Kristo. Tuwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili kwa kutusingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yetu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.     Mungu Baba yetu, kwa rehema zake nyin...

TUACHANE NA UTOTO, ILI KUUKULIA WOKOVU.

TUACHANE NA UTOTO, ILI KUUKULIA WOKOVU. Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu katika Kristo Yesu.     Tukiangalia maandiko, tunaona kuna kuzaliwa kiroho na kuna ukuaji. Na ukuaji kiroho inaonyesha kabisa ni kwa ulaji wa neno la Mungu. Hivyo basi kama watoto wachanga tuliozaliwa sasa tuyatamani maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo tupate kuukulia wokovu, ikiwa tumeonja ya kwamba Bwana ni mwenye fadhili.     Ukuaji wa kiroho unapaswa kukamilika kufikia ukomavu wa kiroho. Tunahuburi habari za Kristo, tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo.     Kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo, kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu na huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe. Na tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, mtu awe mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo. T...

JE, NI NANI ANAPATA UZIMA WA MILELE?

JE, NI NANI ANAPATA UZIMA WA MILELE? Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu katika Kristo Yesu.     Yeye aliye naye Mwana  wa Mungu, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima. Ushuhuda wa Mungu ni kwamba amemshuhudia Mwanawe. Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake asiyeamini huo ushuhuda, amemfanya Mungu kuwa mwongo. Na huo ushuhuda ni kwamba Mungu alitupa uzima wa milele, na uzima huu umo katika Mwanawe.     Amwaminiye Mwana wa Mungu yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia. Amwaminiye hahukumiwi, bali asiyemwamini amekwisha kuhukumiwa kwa kutoliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. Roho wa Mungu anashuhudia na roho zetu kuwa sisi tu watoto wa Mungu. Mungu aliupenda ulimwengu na akamtoa mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye awe na uzima wa milele. 1 Yohana 5:9-12, Yohana 3:36,18, Warumi 8:16, Yohana 3:16.

TUWE WATENDAJI WA NENO.

TUWE WATENDAJI WA NENO. Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu katika Kristo Yesu.     Imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la Kristo. Imani hukua kwa kusikia neno la Kristo kila wakati, usiku na mchana, bila kuchoka, na kulitenda neno. Hivyo basi, tuweke mbali uchafu wa kila namna, na kupokea lile neno lipandwalo ndani yetu ili kuokoa roho zetu; na tuwe watendaji wa neno, wala si wasikiaji tuu, huku tukidanganya nafsi zetu. Na imani bila matendo imekufa.      Maana ukiwa ni msikiaji wa neno na si mtendaji, unafanana na mtu yule anayejiangalia uso wake kwenye kioo; hujiangalia kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo. Hivyo, yeye ajuaye kutenda mema, na hayatendi, kwake huyo ni dhambi. Asikiaye hayo maneno ya Kristo asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu alijejenga nyumba yake juu ya mchanga; mvua ikinyesha, na nyumba hiyo ikapigwa na mafuriko na upepo mkali ikaanguka, tena anguko lake likawa kubwa. Hiv...

JE, AMRI YA KIFO ILITEKELEZWAJE KWA ADAMU?

JE, AMRI YA KIFO ILITEKELEZWAJE KWA ADAMU? Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu katika Kristo Yesu.     Mungu akasema, kwa sababu huyu mtu amejua mema na mabaya, na amekuwa kama mmoja wetu, asije tena akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala akaishi milele; akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi upande wa masharikiwa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima. Akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa.     Hivyo, mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu. Basi kwa jinsi hiyo Mungu aliupenda ULIMWENGU kiasi cha kumtoa mwana wake pekee, mpendwa, ili KILA AMWAMINIYE asipotee, bali awe na uzima wa milele. Mungu amemtuma Mwanawe ili tupate uzima wa yeye, na kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu. Si kwamba sisi tulimpenda, bali yeye alitupenda sisi. Mwanzo 3:22,24,23, Warumi 6:23, Yohana 3:16 & ...

JE, NI NANI ALIYELETA KIFO KWA WANADAMU?

JE, NI NANI ALIYELETA KIFO KWA WANADAMU? Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu katika Kristo Yesu.     Kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi. Adamu alionywa matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya asile, kwa maana siku atakapokula matunda ya mti huo atakufa hakika. Baada ya Adamu kutotii maagizo aliyopewa, aliambiwa atairudia ardhi, ambayo katika hiyo alitwaliwa; kwa maana yu mavumbi, na mavumbini atarudi.     Mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu. Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati. Lakini ashukuriwe Mungu atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Warumi 5:12, Mwanzo 2:17, Mwanzo 3:19, Warumi 6:23,  1 Wakorintho 15:56-57

JE, IMANI PEKE YAKE ITAMWOKOA MTU?

JE, IMANI PEKE YAKE ITAMWOKOA MTU? Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu katika Kristo Yesu.     Mtu akisema anayo imani, aonyeshe imani yake kwa njia ya matendo yake; maana isipokuwa na matendo imekufa nafsini mwake. Mtu anaamini ya kuwa Mungu ni mmoja, atenda vema, ila na mashetani nao wanaamini na kutetemeka.     Ibrahimu alihesabiwa kuwa ana haki kwa matendo alipomtoa mwanawe juu ya madhabahu, na hapa tunaona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, ya kwamba imani ile ilikanilishwa kwa njia ya matendo yale. Mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake. Mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa. Si kila amwambiaye Kristo Yesu, Bwana , Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni, ila yeye afanyaye mapenzi ya Mungu Baba yetu aliye mbinguni. Yakobo 2:14-26, Mathayo 7:21.

JE, MTU ANAWEZA KUOKOLEWA BILA IMANI?

JE, MTU ANAWEZA KUOKOLEWA BILA IMANI? Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu katika Kristo Yesu.     Tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na tuwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema ambayo tunasimama ndani yake, na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu. Tunahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu, ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani ya damu yake. Hivyo mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria.     Mwenye haki wa Mungu ataishi kwa imani, ila akisitasita roho yake haitakuwa na furaha naye. Sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali miongoni mwa walio na imani ya kutuokoa roho zetu. Na ni dhahiri kuwa, hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria. Pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba ye...

JE, MUSA ALIMWAMINI KRISTO?

JE, MUSA ALIMWAMINI KRISTO? Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu katika Kristo Yesu.     Kwa imani Musa alipozaliwa, alifichwa miezi mitatu na wazazi wake bila kuogopa amri ya mfalme; na kwa imani alipokuwa mtu mzima alikataa kuitwa mwana wa binti Farao, akiona ni afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa muda; akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri, kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo. Kwa imani hakuogopa ghadhabu ya mfalme, akatoka Misri, maana alistahimili kama amwonaye yeye asiyeonekana.     Tusiutupe ujasiri wetu maana una thawabu kuu, tukiwaonea huruma wale walio katika vifungo, na tukikubali kwa furaha kunyang'anywa mali zetu, tukijua nafsini mwetu mna mali iliyo njema zaidi, idumuyo. Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao; tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu, ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa ...

TAFAKARI NENO LA MUNGU MCHANA NA USIKU.

TAFAKARI NENO LA MUNGU MCHANA NA USIKU. NEEMA NA IWE KWENU, NA AMANI, ZITOKAZO KWA MUNGU BABA YETU KATIKA KRISTO YESU.     TAFAKARI NENO LA KRISTO (NENO LA BABA) MCHANA NA USIKU, NA UTENDE SAWASAWA NA MANENO YAKE, NDIPO UTAKAPOIFANIKISHA NJIA YAKO NA KUSITAWI SANA. UWE HODARI NA MOYO WA USHUJAA, USIOGOPE WALA USIFADHAIKE, MAANA MUNGU BABA YAKO YU PAMOJA NAWE KILA UENDAKO, KATIKA KRISTO YESU. HAPATAKUWA NA MTU WA KUSIMAMA MBELE YAKO SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO, MAANA HATAKUPUNGUKIA WALA HATAKUACHA.     KRISTO YESU HAKUJA KUTANGUA TORATI NA MANABII, BALI KUTIMILIZA. NA AKASEMA, MPAKA MBINGU NA NCHI ZITAKAPOONDOKA, YODI MOJA WALA NUKTA MOJA YA TORATI HAIONDOKI, HATA YOTE YATIMIE. MTU YO YOTE ATAKAYEVUNJA AMRI MOJA KATIKA HIZI ZILIZO NDOGO, NA KUFUNDISHA WATU HIVYO, ATAITWA MDOGO KABISA KATIKA UFALME WA MUNGU. KRISTO NI MWISHO WA SHERIA, ILI KILA AAMINIYE AHESABIWE HAKI. LILE NENO LA IMANI LIHUBIRIWALO LIWE KARIBU NAWE, KATIKA KINYWA CHAKO NA KATIKA MOYO WAKO. ...

MTAFUTE BWANA KWA MOYO WAKO WOTE.

MTAFUTE BWANA KWA MOYO WAKO WOTE. Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu katika Kristo Yesu.     Utamtafuta na kumuona, utakapomtafuta kwa moyo wako wote. Maana anajua mawazo anayokuwazia wewe, asema BWANA, ni mawazo ya amani, wala si mabaya, kukupa wewe tumaini siku zako za mwisho. Utamwita, utakwenda na kumuomba, naye atakusikiliza na ataonekana kwako. Naye atakupa moyo, umjue ya kuwa yeye ni BWANA; nawe utakuwa mtu wake, naye atakuwa Mungu wako; kwa maana utamrudia kwa moyo wako wote.     Ombeni nanyi, mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa. Mwaminini Mungu, na yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu. Na mkiomba lo lote kwa jina la Kristo Yesu, hilo atalifanya yeye Kristo, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Yeremia 29:11-13, Yeremia 24:7, Mathayo 7:7, Marko 11:22, Yohana 14:13.

UPENDO WA MUNGU KWETU.

UPENDO WA MUNGU KWETU.     Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu katika Kristo Yesu.     Mungu, Baba yetu aliye mbinguni, alionyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu. Tulipokuwa adui, tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake na twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye sasa tumepokea huo upatanisho.     Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele; na hakumtuma Mwana ulimwenguni kuhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu.    Wapenzi, na tup...

VINAVYOONEKANA NI VYA MUDA. VISIVYOONEKANA NI VYA MILELE.

VINAVYOONEKANA NI VYA MUDA. VISIVYOONEKANA NI VYA MILELE. Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu katika Kristo Yesu.                       Ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. Na Mungu, Baba yetu wa mbinguni atujalie kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, tufanywe imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake, katika utu wa ndani.     Dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana; Hivyo basi, tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele. Tuyahesabu mateso ya wakati huu wa sasa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu.     Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Kwa imani twajua ya kuwa ulimwengu uli...

MCHUNGAJI WANGU MWEMA

MCHUNGAJI WANGU MWEMA . 1. BWANA NDIYE MCHUNGAJI WANGU, SITAPUNGUKIWA NA KITU:   Bwana wetu Yesu Kristo ndiye mchungaji mwema; maana mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake; humwona mbwa mwitu anakuja, huwakimbia na kuwaacha kondoo, na mbwa mwitu huwakamata na kuwatawanya. Tulio wake Kristo Yesu anatujua, na tulio wake tunamjua, kama Baba amjuavyo yeye, na yeye amjuavyo Baba, na ameutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.     Kristo Yesu, alitukanwa, aliteswa, akajikabidhi kwake ahukumuye kwa haki. Akazichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, ili tuwe wafu kwa mambo ya dhambi, na tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake tumepona. Tulikuwa tunapotea kama kondoo, lakini sasa tumemrudia Mchungaji na Mwangalizi wa roho zetu. Mchungaji mwema huacha wale kondoo tisii na kenda na kwenda kumtafuta yule mmoja aliyepotea, maana ni furaha mbinguni kwa mmoja mwenye dhambi atubuye, ku...

JE, WAMWAMINIJE YEYE WASIYEMSIKIA?

JE, WAMWAMINIJE YEYE WASIYEMSIKIA?     Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu.     Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!     Lakini si wote walioitii ile habari njema. Kwa maana Isaya asema, Bwana, ni nani aliyeziamini habari zetu? Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako, na ni lile neno la imani tulihubirilo.     Hivyo basi, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na ukaamini moyoni mwako ya kuwa Mungu Baba yetu wa Mbinguni alimfufua katika wafu utaokoka. Maana kwa moyo mtu huamini na kupata haki, na kwa kinywa mtu hukiri na kupata wokovu.     Sasa basi kumwamini Kristo Yesu usiyemsikia huja kwa kusoma neno la ...

NENO LA UJUMBE LA MUNGU.

NENO LA UJUMBE LA MUNGU.     Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu.     Mnapopata neno la ujumbe la Mungu, mnalolisikia kwa watumishi wa Mungu au kwa kusoma maandiko, mlipokee si kama neno la mwanadamu, bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kweli kweli, na litendavyo kazi ndani yenu ninyi mnaoamini. Injili aliyoihuiri Mtume Paulo, aliwajulisha sio ya namna ya kibinadamu, kwa kuwa hakupokea kwa mwanadamu wala hakufundishwa na mwanadamu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo. Mungu ametuchagua tangu mwanzo tupate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli aliyotuitia kwa injili, ili kuupata utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo. Basi ndugu, msimame imara kwa kuyashika mapokeo ya kweli mnayofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wa mitume. Basi mlipokee lile neno kwa uelekevu wa moyo, mkiyachunguza maandiko kila siku, muone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo. 1 Wathesalonike 2: 13, Wagalatia 1:11, 2 Wathesalonike 2:13, Matendo ya M...

NENO LETU NA KUHUBIRI KWETU.

NENO LETU NA KUHUBIRI KWETU.     NEEMA NA IWE KWENU, NA AMANI, ZITOKAZO KWA MUNGU BABA YETU.     NENO LETU NA KUHUBIRI KWETU KUSIWE KWA MANENO YA HEKIMA YENYE KUSHAWISHI AKILI ZA WATU, BALI KWA DALILI ZA ROHO NA ZA NGUVU, ILI IMANI YA WATU ISIWE KATIKA HEKIMA YA WANADAMU, BALI KATIKA NGUVU ZA MUNGU.     TUNENE HEKIMA YA MUNGU KATIKA SIRI, ILE HEKIMA ILIYOFICHWA, AMBAYO MUNGU ALIIAZIMU TANGU MILELE, KWA UTUKUFU WETU, AMBAYO WENYE KUITAWALA DUNIA HII HAWAJUI HATA MMOJA, MAANA WANGEJUA WASINGEMSULUBISHA BWANA WA UTUKUFU. NI MAMBO AMBAYO JICHO HALIKUYAONA, WALA SIKIO HALIKUYASIKIA, WALA HAYAKUINGIA KATIKA MOYO WA MWANADAMU, AMBAYO MUNGU ALIWAANDALIA WAMPENDAO.     MAMBO HAYO MUNGU AMETUFUNULIA SISI KWA ROHO, MAANA ROHO HUCHUNGUZA YOTE HATA MAFUMBO YA MUNGU. MTU WA ROHONI HUYATAMBUA YOTE, WALA YEYE HATAMBULIWI NA MTU.   1 WAKORINTHO 2.

MAOMBI YA KRISTO YESU KWA AJILI YA WALIO WAKE (WA KRISTO).

MAOMBI YA KRISTO YESU KWA AJILI YA WALIO WAKE (WA KRISTO). Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu.     Maneno hayo aliyasema Yesu; akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe; kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele. Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako wamelishika.     Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako; Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu.     Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao w...

KUJUA SIRI YA MUNGU.

KUJUA SIRI YA MUNGU.     NEEMA NA IWE KWENU, NA AMANI, ZITOKAZO KWA MUNGU BABA YETU.     TUFARIJIKE MIOYO YETU, TUKIUNGANISHWA KATIKA UPENDO, TUPATE UTAJIRI WOTE WAKUFAHAMU KWA HAKIKA, NA TUPATE KUJUA SIRI YA MUNGU, YAANI NDANI YA KRISTO HAZINA ZOTE ZA HEKIMA NA MAARIFA ZIMESITIRIKA.     MTU ASIJE KUWADANGANYA  KWA MANENO YA KUWASHAWISHI.     KRISTO AKAE MIOYONI MWETU KWA IMANI TUKIWA NA SHINA NA MSINGI KATIKA UPENDO; ILI TUPATE KUFAHAMU PAMOJA NA WATAKATIFU WOTE JINSI ULIVYO UPANA, NA UREFU NA KIMO NA KINA, NA KUUJUA UPENDO WAKE KRISTO, UPITAO UFAHAMU KWA JINSI ULIVYO MWINGI, TUPATE KUTIMILIKA KWA UTIMILIFU WOTE WA MUNGU.     MWENYE MWILI AWAYE YOTE ASIJE AKAJISIFU MBELE ZA MUNGU, BALI KWA YEYE TUMEKUWA KATIKA KRISTO YESU, ALIYEFANYWA HEKIMA ITOKAYO KWA MUNGU, NA HAKI, NA UTAKATIFU, NA UKOMBOZI, ILI KAMA ILIVYOANDIKWA, YEYE AONAYE FAHARI NA AONE FAHARI JUU YA BWANA.     SIRI ILE ILIYOFI...

JE, INJILI ILIHUBIRIWA ZAMANI, KAMA WAKATI WA IBRAHIMU?

JE, INJILI ILIHUBIRIWA ZAMANI, KAMA WAKATI WA IBRAHIMU? Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani, lilimhubiri Ibrahimu habari njema zamani, kusema, Katika wewe Mataifa yote watabarikiwa. Wagalatia 3:8 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Kama Ibrahimu alivyomwamini Mungu wa mbinguni akahesabiwa haki, hivyo tufahamu kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu, nao hubarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa na imani. Andiko lilimhubiria Ibrahimu habari njema zamani, kwamba katika yeye Mataifa yote watabarikiwa, sababu liliona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani. Na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa. nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa. Mwanzo 12:3 Naam, na manabii wote tangu Samweli na wale waliokuja baada yake, wote walionena, walihubiri habari za siku hizi. Ninyi m...

JE, MUNGU AMEWEKA MIPANGO MINGAPI YA WOKOVU?

JE, MUNGU AMEWEKA MIPANGO MINGAPI YA WOKOVU? Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. Matendo ya Mitume 4:12 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Ameweka mpango mmoja tuu, nao ni wanadamu kuokolewa kwa jina moja, nalo ni jina la Kristo Yesu. Yusufu, mwana wa Daudi aliambiwa na malaika katika ndoto kuwa, asihofu na amchukue Mariamu mkewe, maana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu; atazaa mwana na wamwite jina lake Yesu, maana ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.

JE, NI HESHIMA KIASI GANI INAYOSTAHILI KWA KRISTO?

JE, NI HESHIMA KIASI GANI INAYOSTAHILI KWA KRISTO? ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba aliyempeleka. Yohana 5:23 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Tunavyomheshimu Baba yetu aliye mbinguni ndivyo tanatakiwa kumheshimu Mwana, yaani Kristo Yesu. Kristo Yesu hakutenda neno mwenyewe ila lile ambalo Baba analitenda, tena amempa yeye hukumu yote. Tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina, ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba. Kila amkanaye Mwana, hanaye Baba; na amkiriye Mwana anaye Baba pia. Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma. Luka 10:16

JE, KANISA LA KIKRISTO LIMEJENGWA JUU YA MSINGI GANI?

JE, KANISA LA KIKRISTO LIMEJENGWA JUU YA MSINGI GANI? Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Waefeso 2:20 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Bwana, MUNGU, asema hivi, Tazama, naweka jiwe katika Sayuni, liwe msingi, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni lenye thamani, msingi ulio imara. Katika Kristo jengo lote linaunganishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana, na katika yeye tunajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho. Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Mathayo 16:16,18

HALAFU MWILI WA MTU HUWA NINI?

HALAFU MWILI WA MTU HUWA NINI? Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; 1 Wakorintho 6:19 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Tumekuwa hekalu la Mungu, na Roho wa Mungu anakaa ndani yetu. Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo, sababu hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo sisi. Maana tulinunuliwa kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani ya Kristo Yesu , hivyo tumtukuze Mungu katika miili yetu. Mlinunuliwa kwa thamani; msiwe watumwa wa wanadamu. 1 Wakorintho 7:23

JE, AHADI ZA MUNGU ZIMEWEKWA ULIMWENGUNI KWA SABABU GANI?

JE, AHADI ZA MUNGU ZIMEWEKWA ULIMWENGUNI KWA SABABU GANI? Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa. 2 Petro 1:4 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Ni ili tupate kuwa washarika wa tabia za Uungu, tukiokolewa na uharibifu uliomo humu duniani unaosababishwa na tamaa. Ametukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Tujitahidi sana kwa upande wetu, katika imani yetu tutie na wema, katika wema wetu maarifa, katika maarifa yetu kiasi, katika kiasi chetu saburi, katika saburi yetu utauwa, katika utauwa wetu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, UPENDO. Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya aj...

JE, MTU AKIKAA NDANI YA KRISTO, ANATAKIWA AENENDE NAMNA GANI?

JE, MTU AKIKAA NDANI YA KRISTO, ANATAKIWA AENENDE NAMNA GANI? Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda. 1 Yohana 2:6 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Twajua tumo ndani yake kwa kulishika neno lake, na katika Kristo, upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Ukisema umemjua wala huzishiki amri zake ni mwongo, wala kweli haimo ndani yako. Kumpenda Mungu ni kwamba tuzishike amri zake wala si nzito. Tujitie nira ya Kristo, tujifunze kwake, kwa kuwa yeye ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nasi tutapata raha nafsini mwetu; kwa maana nira yake ni laini na mzigo wake ni mwepesi. Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. Yohana 15:10 Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo. Yohana 13:15