JE, UTAKUJA WAKATI WATU HAWATAISIKILIZA ILE KWELI KWENYE BIBLIA? Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo. 2 Timotheo 4:3-4 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Kweli ipo, ila watu wataikwepa iliyo kweli na kufuata waalimu makundi makundi kwa hadithi na mafundisho ya uongo. Na ukweli upo, ila umepindishwapindishwa na unaendelea kupindishwapindishwa. Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; Bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa. 1 Timotheo 4:1-7 Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu. 2 Wathesalonike 2:15
KARIBU KWENYE BLOG YENYE TAFAKARI NA MASOMO YA NENO LA MUNGU. MJUE SANA MUNGU ILI UWE NA AMANI; NDIVYO MEMA YATAKAVYOJIA. NENO LAKE ULIWEKE MOYONI MWAKO.